Lyrics: Roma – Hivi Ama Vile Ft. Stamina [New Lyrics]
[Chorus/Hook: Roma & Stamina]
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
[Verse 1: Roma & Stamina]
Stamina: Mimi nampenda uncle Magu
mwokozi wa makapuku.
Roma: Ah mimi ukinikata damu yangu
ni lowasa mtupu,
So wanangu wa ukawa vidole viwili
juu,
Stamina: Hapa kazi tu ikulu
mtapasikia tu,
Roma: Hata nifungwe mimi ni Arsenal
sio Man U,
Stamina: Hamna lolote ndio maana
hamchezi UEFA msimu huu,
Bongo mimi ni Yanga tena vikombe ni
tele,
Roma: Ah wapi wanangu wa simba
piga kelele,
Ah nampenda snura ana bonge la
chura,
Stamina: Mh mm..nampenda shishi
mwanamke sura,
Roma: Ah acha ubishi dogo,
Stamina: Acha ligi,mimi amber lulu
ndio mkali,
Roma: Mimi Gigy,
Stamina: Eti mziki una team haya
team kiba mko wapi,
Roma: Team hazijengi hata wasafi
wakijenga masaki,
Mimi wema we boya tu unalipi la
kusema?,
Stamina: Mimi zari niko zangu madale
na naishi vyema,
[Chorus/Hook: Roma & Stamina]
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
[Verse 2: Roma & Stamina]
Roma: Mimi mziki ukinishinda mdogo
wangu nitakuwa mkulima,
Stamina: Mimi nitakuwa mfugaji nifuge
vyote vya nchi nzima,
Roma: Lakini kweli nikila ugali si
nitahitaji na nyama?,
Stamina: Basi bifu la wakulima na
wafugaji halina maana,
Roma: Ila Ronaldo mkali ki-soccer
hana mpinzani,
Stamina: Hawezi kumzidi Messi
wakikutana Dimbani,
Kwanza Madrid siwapendi
washanichania mikeka,
Roma: Acha soccer huliwezi ka-bet
kwenye mieleka,
Stamina: Hivi Ney na Madee nani raisi
wa manzese,
Roma: Hata udiwani hawafai,kwanza
mmoja ana kithethe,
Nisha zunguka nchi nzima kila kona
ninashabiki,
Stamina: Acha uwongo hivi ushafanya
show kibiti,
Roma: Madereva tunaleseni makonda
mnatupa loss,
Stamina: Mbona makonda hatuna
vyeti ila tunaaminiwa na boss,
Ila wewe bwege ukimuacha mama
Ivan utapata dhambi,
Roma: Walahi! nishaweka kambi
ninampenda Mange Kimambi,
[Chorus/Hook: Roma & Stamina]
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku
ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku
ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo
ziskia kule,
[Outro: Roma & Stamina]
Roma: Hehehee..Ila mdogo wangu
wewe unapenda sana Ligi wewe,
Yani wewe unaweza ukabisha mpaka
outro wewe,
Kwa mfano mimi kama mimi yani,
mimi nakumbia namkubali Mussa
babas wa babas,
Stamina: Wai…kimpango wako bwana
wewe,
si unajua watu wafupi,afu si unajua
tabaka la morogoro,
Mimi namkubali chief Kiumbe wewee,
Roma: HAHAAA..!
No comments