ROMA_ZIMBABWE (LYRIC)
[Intro]
Wengi mlijiuliza walioniteka ni
maaskari?
Mkanitafuta vituo vyote Cetral hadi
sitaki shari,
Wakasema hawajui nilipo mama
alienda mpaka monjwari,
Daaah!,yakaisari mwachie kaisari,
Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga
na kusali
[Bridge]
Imba roma Imbaaa
Imba roma Imbaaa,
Imba roma Imbaaa,
[Verse 1]
Mungu wa paul ndio mungu wadaudi,
Na ndio mungo wa John Mnaemuita
Yohana wa wayahudi,
Mwanangu alimuuliza mama “Baba
lini atarudi”?,
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru
sinabudi,
Kwa hamu ya kuwa mimi sio tu rapper,
Mimi ni baba wa Familia,
Nawatoto mahitaji nawapa kama
isemavyo biblia,
Kipi bora?Nife mseme nilikufa
kiharakati?,
Siogopi kufa ila nawaachaje
wanaobaki?,
Je! Nani kati yenu mwanangu atampa
malezi?,
wapi atapata mahitaji?,wapi atapata
mapenzi?,
Mama nae wapi atapata mahitaji na
malezi?,
Na report ya upelelezi vipi akiiteka
mtekaji?,
Je! Kaburi langu mtalipalilia majani,
Nimeumwa hamjakuja
kuniona,mnangoja mje msibani?,
Nilipokuwepo sikuwa najua hii
sanne,hii saanane,
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu
zangu tuonane,
Nimechapwa Mijeledi nimevunjwa bila
huruma,
Asante mliopaza sauti nimeiona nguvu
ya umma,
Sikutatu nimefungwa macho,mikono
imefungwa nyuma,
Chorus/Hook
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
[Bridge]
Imba roma Imbaaa,
Oo,Eee mama(sema baba wewe)
Verse 2
Nasimama nanaunga hoja kwenye
uchumi wa Viwanda,
Nanasi linauza msoga,tikiti linaoza
shamba,
Walioniteka hawakuja na noah,Ni
uvumi na visanga,
ila kutekanateka huu ni uhuni wa
kishamba,
Weka Bunduki chini si tubishane kwa
hoja,
Maana sote lengo letu kuijenga
Tanzania moja,
Mi-sikuona nyota kwa shoulder,Ila
najua wewe ni soldier,
(Inshallah)Ulikuja mwenyewe ama
ulipewa order(hewallah),
Lyrics by skiizat
Aminini siku hazigandi,wewe ni yanga
mimi simba,
Kwa mpinzani sio dhambi,
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani,
Simba akichukua kombe sijui atapona
nani,
Na kuna mbunge alisema eti
nimemtukana mkuu,
Utahukumiwa na mkono wa
Mungu,kumshtakia aliye juu,
Kwanza lini,na kwanini mimi
nimtukane mjomba,
Umepewa gari ya wagonjwa,mi Tanga
wananijalia bomba,
Mimi mbarikiwa na nikifa nitaketi
kuume kwa baba,
na ni mtu wa watu that is
why,lilisimama bunge la bajeti,
Kunijadili mtanzania kuwa makini pia
makinikia nayatungia,
Mapini Piyaa,
Nilitabiri utaitwa Raisi kipindi unaitwa
waziri,
Japo maisha sio rahisi japo pongezi
unastahili,
waliosadiki roma ataonekana kabla ya
jumapili,
God bless imetimia injili nilio itabiri,
Chorus/Hook
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Nakwendaaa Zimbabwe(Zimbombo
Iyelele mama we),
Outro
Imba roma(ee ee roma),
Zimbomboo we simama(ee ee roma),
sema baba wewe(ee ee roma),
iyelelel mama wewee(zimbombo we
simama),
watakwenda,uko zimbabwee,
ee ee roma(iyelele mama wewee)
No comments