Kwa Picha: Meli ya kivita ya Marekani USS Fitzgerald ilivyoharibiwa
Picha uharibifu uliotokea baada ya meli ya kivita ya Marekani USS Fitzgerald kugongana na meli ya mizigo
Manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya kubeba mizigo mwendo wa saa nane unusu usiku wa manane saa za Japan Jumamosi.
Ajali hiyo ilisababisha maji kufurika katika meli hiyo ya Marekani. Wanabaharia saba walitoweka.
Meli hiyo, ikiwa imeharibiwa, ilirejea pole pole ikisaidiwa na boti kadha hadi katika kambi ya majeshi ya Marekani Yokosuka
Haijabainika ilitokea vipi meli hiyo ya kivita, ambayo ni moja ya meli zenye mitambo ya kisasa zaidi duniani, ikagongana na meli hiyo ya mizigo.
Watu watatu, akiwemo kamanda mkuu wa meli hiyo, walilazwa hospitalini.
Ajali hiyo ilitokea eneo lenye maji matulivu, na hali ya anga ilikuwa nzuri.
Meli ya mizigo iliyogongana na meli hiyo ya Marekani, ACX Crystal ambayo imesajiliwa Ufilipino, haikuharibiwa sana
ACX Crystal iliendelea na safari yake hadi Tokyo
Meli hiyo ya Ufilipino ilikuwa na uzani karibu mara tatu ukilinganisha na meli hiyo ya Marekani.
Ramani ya safari ya meli hiyo ya Ufilipino na eneo ambalo meli hizo mbili ziligongana.
No comments