Habari Picha: Shambulio la gari Las Ramblas, Barcelona
Picha za kutoka eneo ambapo gari lilivurumishwa kwenye umati eneo la kitalii la Las Ramblas mjini Barcelona, Uhispania. Watu 13 wamefariki.
Watu takriban 13 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya gari kuvurumishwa kwenye umati wa watu katika eneo la kitalii la Las Ramblas, Barcelona.
Polisi wamekuwa wakimsaka mshambuliaji ambaye inaaminika alitoroka kutoka eneo hilo kwa miguu.
Watoto waliojawa na wasiwasi walisaidiwa kukimbilia eneo salama, operesheni ya kumsaka mshambuliaji ilipokuwa ikiendelea.
Polisi waliondoa wengi wa watu katikati mwa jiji baada ya shambulio hilo kutokea.
Watu wengi walitafuta hifadhi katika migahawa na baa zinazopatikana Las Ramblas.
Mchuuzi wa puto hizi aliziacha katika eneo la Plaça Catalunya na kukimbilia usalama.
Waliokuwa eneo hilo walifarijiana baada ya kufika maeneo salama.
Gari lililotumiwa kutekeleza shambulio hilo limebururwa na kuondolewa eneo hilo na polisi.
Walioshuhudia wameeleza jinsi gari hilo lilivyoendeshwa makusudi kuwagonga watu wengi kwenye eneo wa kutumiwa na wapita njia.
Maafisa wa polisi sasa wanafanya uchunguzi eneo hilo.
Polisi wa Uhispania baadaye walisema walikuwa wamewaua washukiwa watano wa ugaidi katika mji wa Cambris na kuzuia shambulio la pili la kutumia magari.
Gari hili, lililokuwa na washukiwa Cambrils, liliondolewa eneo hilo Ijumaa asubuhi.
Licha ya shambulio hilo, maduka yalifunguliwa Las Ramblas Ijumaa asubuhi.
Watu wameanza kutoa heshima zao kwa waliofariki Las Ramblas
No comments