Samaki wanaogeukia pombe ili kuishi
Wanasayansi wamebaini siri ya samaki wa dhahabu jinsi wanavyoweza kuishi chini ya maziwa yaliyofunikwa na barafu.
Watafiti hao pia wamebaini kwa nini samaki na ni jinsi gani samaki hao hugeuza asidi ya lactic kwenye miili yao kuwa pombe, kama ya njia ya kuwawezesha kuendelea kuwa hai.
Baadhi ya samaki hao waligunduliwa kuwa na viwango vya juu vya pombe kushinda kiwango dereva anachostahili kuwa nacho kwenye damu anapoendesha gari katika nchi nyingi.
Watafiti hao wamesema utafiti huo unaweza kuwasaidia kufanya utafiti zaidi kuhusiana na madhara yanayotokana na pombe kwa binadamu.
Wanasayansi wamekuwa anafahamu kuhusu uwezo wa kipekee wa samaki hao wa dhahabu kuweza kuishi maeneo yenye hali ngumu ya kimazingira na wenzao wa baharini aina ya Crucian Carp tangu miaka ya 1980.
Ingawa binadamu na wanyama wengine wenye uti wa mgongo hufariki muda mfupi baada yao kukosa hewa ya okisejeni, samaki hawa wana uwezo wa kuishi katika mazingira hayo ya barafu kwa miezi kadhaa katika bahari kaskazini mwa bara Ulaya.
Watafiti hao wamebaini jinsi wanyama hao hutumia mbinu maalum kuwawezesha kuendelea kuishi katika mazingira hayo.
Kwa wanyama wengi kuna aina moja ya protini ambayo hutumiwa kuelekeza wanga (kabohaidreti) kwenye mitochondria, viungo vinavyotumiwa kuzalisha kawi kwenye seli.
Iwapo hakuna hewa ya okisejeni, kutumiwa kwa wanga kuzalisha nishati huzalisha asilidi aina ya alctic ambayo samaki hawa huwa hawawezi kuiondoa mwilini.
Asidi hiyo huua kiumbe baada ya dakika chache.
Kwa bahati nzuri, samaki hao wa dhahabu wamebadilika na kuwa na seti ya pili ya protini ambayo inaweza kufanya kazi hata okisjeni ikiwa haipo na huibadilisha asidi ya lactic kuwa pombe, ambayo baadaye hutolewa mwilini kupitia kwenye yavu yavu za samaki hao.
"Njia hii ya pili huanza kutumiwa tu iwapo hakuna okisjeni," mwandishi Dkt Michael Berenbrink kutoka chuo kikuu cha Liverpool huko Uingereza, aliambia BBC
Barafu huwafunikia samaki hao na kuwazuia kupata hewa, kwa hivyo wanapokuwa kwenye kidimbwi kilichofunikwa na barafu samaki hao wa dhahabu huvuta hewa yote ya okisjeni na kuibadilisha kuwa pombe.
Endapo wanakuwa kwenye barafu, na eneo ambayo halina hewa ya kutosha kiwango cha pombe huongezeka kwenye samaki hao.
Licha ya kwamba samaki hao wanaweza kujaza pombe kwenye yavu yavu zao, si pombe inayowaua mwishowe.
Iwapo majira ya baridi yataongezeka na baridi kuzini, huwa wanaishiwa na mafuta ya kuzalisha nishati ambayo huwa kwenye ini na mwishowe hufariki.
Watafiti wanasema kuna mafunzo muhimu yanastahili kuangaziwa kuhusiana na jinsi samaki hao wanavyoweza kuzalisha jeni aina mbili ambazo zina uwezo wa kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kawaida, na pia kuwafaa hali ikibadilika.
"Uzalishaji wa ethanol huwasaidia samaki aina ya Crucian Carp kuwa samaki wa kipekee wanaoweza kuishi katika mazingira hayo makali na kujiepusha na maadui wengi," amesema mwandishi mkuu wa utafiti huo Dkt. Cathrine Elisabeth Fagernes kutoka chuo kikuu cha Oslo, Norway.
Wanasayansi pia wamefanya hesabu kubaini ni muda gani unaoweza kutumika kuunda kileo kutoka kwa 'kinyesi' cha samaki hao.
Kujaribu kupata pombe ya kunywa kutoka kwa samaki hao ni kibarua kigumu
"Ukiwaweka ndani ya gilasi ya bia na kuifunika kabisa, itawachukua siku 200 kufikia kiwango cha ukali wa pombe wa asilimia nne," anasema Dkt Berenbrink.
Katika mazingira ya kawaida, hilo haliwezi kutendeka.
Utafiti huo umechapishwa kwenye jarida la kisayansi la Scientific Reports.
No comments