UN yataka mapigano kusitishwa Syria kupisha misaada
Raia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu
Umoja wa Mataifa umetoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka.
Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati maeneo hatari duniani na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa mwanya kwa raia kutoroka katika eneo hilo.
Amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita.
Hata hivyo idadi hiyo ya raia wapatao 25,000 kwa wamekwama ndani ya mji huo huku kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya anga kwa juma moja lililopita.
Ragga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani
Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangua mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi june mwaka huu.
Wapiganaji wa IS wanatuhumiwa na umoja wa mataifa kwamba wanatumia raia kama kinga yao katika mapigano hayo.
Marekani na Muungano wa vikosi vya Syria, Kiarabu na Kikurdi wanajaribu kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic state.
No comments