Kichanga Kilichojeruhiwa na Polisi Nchini Kenya Chafariki
Mtoto Samantha Pendo mwenye umri wa miezi sita ambaye alijeruhiwa na maafisa wa polisi nchini Kenya walipovamia nyumba yao, amefariki dunia akiwa hospitali.
Daktari Sam Oula wa Hospitali ya Agakhan ambapo mtoto huyo alilazwa alikiri kumpokea mtoto huyo siku ya Jumamosi, na kusema alikuwa katika hali mbaya wakati wakimpokea hospitali hapo.
Baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Joseph Abanja alitoa taarifa za kifo hicho, na kusema kuwa wakati tukio linatokea mtoto wake alikuwa amebebwa na mama yake na walikuwa ndani ya nyumba, na ndipo polisi walitokea na kurushia bomu la machozi, kasha kuwavamia wakiwa ndani na kumpiga mke wake na kuanguka chini, alipoangua ndipo alipomuumiza mtoto kwa kuwa aliangukia kichwa.
Taarifa zinasema polisi hao walikuwa wakiwatawanya watu ambao walikuwa wanaandamana wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8 mwaka huu.
No comments