• Breaking News

    NOWMAA:Fid Q Amtaka Ali Kiba Wafanye Remix Nyingine ya FRESH


    Nyota wa muziki wa hiphop kutoka Mwanza, Fid Q amefunguka namna Diamond alivyomshawishi hadi kumuweka kwenye 'Fresh Remix' ngoma ambayo imepaka upya rangi ya mng'ao Bifu la Ali Kiba na Diamond....

    Mkali huyo wa michano amesema Diamond alimuahidi kumshangaza katika verse yake na kukiri wazi kuwa Aliipenda mistari ya CEO huyo wa WCB .

    "Alinipigia simu Tale akaniambia Fid eeh nipo na Mond hapa anataka aongee na wewe nikamwambia poa mpe nimsikie, (Diamond) Kaka vipi bhana hii fresh nimeielewa kama vipi tufanye remix mzee halafu mimi nitaku'suprise kwa kuchana humu...Nikamuambia chana halafu unitumie. Akachana ile verse then akanitumia alivyonitumia ile verse niliipenda ukizingatia Diamond ni number 1 Artist in the country (Tz) anafahamika kwa uimbaji halafu akaamua kuchana hii ni baraka kwa muziki wa hiphop na rap kwa ujumla" alisema Fid Q.

    Kuhusu ngoma yake kutumika kuchochea bifu la mafahari hao wawili Diamond na Alikiba
    Fid Q amesema

    "Mimi siamini kama nimetumika kama daraja mimi sio team Diamond wala sio Team Kiba moja ya ndoto zangu ni kukutanisha hawa watu wawili waweze kufanya kazi pamoja tuondoe maswala ya u'team tuweze kutengeneza wakina Diamond na Alikiba wengine! hizo ndio ndoto zangu" .

    Katika hatua nyingine star huyo wa 'Fresh' amesema yupo tayari kufanya Fresh Remix nyingine na Alikiba kama msanii huyo akihitaji kufanya .

    No comments