Afrika kusini yaweka 'tahadhari' mipakani kumzuia Bi Mugabe
Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe
Maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wametoa tahadhari dhidi ya Mkewe rais Mugabe katika mipaka ya taifa hilo , waziri wa polisi nchini humo amesema.
Ametuhumiwa kwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .
Polisi wanatariaji kwamba Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 52 alipaswa kujiwasilisha mbele yao siku ya JUmanne lakini akakataa kufanya hivyo.
Bi Grace mugabe kwa sasa hajulikani yu wapi lakini inaaminikwamba bado yupo Afrika Kusini.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amewasili nchini Afrika Kusini kwa kikao cha viongozi wa mataifa ya Afrika Kusini SADC unaotarajiwa kuanza siku ya Ijumaa.
Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Waziri wa polisi Fikile Mbalula alisema: Sisi polisi wa Afrika Kusini tayari tumeweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano, wakili wa Afrika Kusini Gerrie Nel aliyefanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar PIstorius anamuunga mkono mwanamke anayemtuhumu bi Mugabe kwa kumpiga, Gabriela Engels.
Bwana Nel sasa anashirikiana na kundi la Afriforum ambalo linapigania haki za Afrikaners nchini Afrika Kusini.
Kundi hilo limesema kuwa iwapo polisi watashindwa kuchukua hatua katika kesi hiyo basi litamshtaki bi Mugabe.
Pia limesema kuwa litakabiliana na hatua yoyote ya kumpatia kinga ya kidiplomasia bi Mugabe.
Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.
''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo..
No comments