Wahindi Wekundu; wanaotembea bila nguo, walaji wa nyani
KATIKA mfululizo wa makala za safu hii, tuliwaeleza kuhusu watu weusi wa Papua New Guinea ambao licha ya kukaa bila kuvaa nguo walikuwa na tabia ya kutisha ya kula nyama za watu. Baada ya kuwasimulia simulizi ndefu juu ya watu hao, tukaenda Ethiopita ambako tuliwaona na kuwachambua watu wa kabila la Bodi ambao nao walikuwa wakitembea bila nguo na kupenda vitambi, kwamba bila kitambi, mwanaume anadharaulika.
Hivyo ikawa inawabidi wavulana kuwekwa katika nyumba maalum ili ‘kuotesha’ vitambi kisha kushindanishwa na mshindi kuzawadiwa ng’ombe na kuwa rahisi kwake kupata mke. Lakini utaratibu wa zawadi ukaboreshwa, washindi wakawa wanapewa pia kombe kutokana na kuwa wanene.
Makabila yote hayo ni ya watu wenye asili ya Afrika, kwa kuwa walikuwa weusi tii! Leo nakuletea Wahindi Wekundu wa Kabila la Huarorani, hawa wanaishi kwenye misitu ya Amazoni huko Jamhuri ya Ecuador. Nchi hii ipo kaskazini mashariki mwa Bara la Amerika ya Kusini na inapakana na nchi ya Colombia iliyo kaskazini mwa nchi hiyo na kwa upande wa mashariki inapakana na Bahari ya Pasifiki.
Nchi hiyo yenye mji mkuu wake uitwao Quito, inakaliwa na watu wanaojulikana kama
shughuli zao bila wasiwasi wowote. Watu hawa, huko nyuma walikuwa wakiishi kwa kutegemea uwindaji tu na kula matunda ya porini, lakini kwa miaka 40 sasa wamekuwa wakijiingiza katika shughuli za kilimo japokuwa uwindaji hawauachi.
Kazi ya kuwinda hufanywa na wanaume na huanza kufundishwa vijana baada ya kubalehe. Kazi hiyo hufanywa kwa kutumia silaha za jadi ambazo ni upinde na mishale pamoja na mikuki. Lakini pia wapo Wahuarorani wanaotumia mitego ya kienyeji kunasa wanyama wanaowataka. Kabila hili hupendelea sana kula nyama ya nyani na wanasema ni tamu sana kuliko nyama nyingine.
Wanyama hao huwindwa kwa kutumia mishale au vijiti maalum vyenye sumu. Nyani wanapoona watu, hukimbilia juu ya miti na watu hao huwa na vijiti maalum ambavyo huwa wamevipaka sumu na kuwapulizia. Vijiti hivyo ambavyo huwekwa kwenye mwanzi maalum humpata nyani na kumchoma, hivyo ile sumu kumuingia mnyama huyo na kufa.
“Hii sumu haitudhuru tunapokula nyama ya nyani aliyekufa kwa sumu. Sumu ikiingia kwenye damu inakosa nguvu ikipikwa kwa sababu ni ya majani fulani ya porini,” alisema mmoja wa wawindaji hao waliozungumza na mwandishi mmoja aliyekwenda kupata habari zao.
Mtu mmoja anaweza kwenda kuwinda nyani na kufanikiwa kuwaua watatu hadi wanne na huliwa kwa njia tofauti, wapo wanaowabanika na wengine huwapika na kuwa mchuzi. Fuatilia simulizi hii ya kweli uone maajabu ya dunia Jumanne ijayo hapahapa!
No comments